Mitazamo ya Daistopia Katika Riwaya Teule za Kiswahili

Authors

  • Martha Nyangweso Syekei Rongo University
  • Carren Nyandiba Senior Lecturer, Department of Language, Linguistics and Literature, Rongo University
  • Silas Owala Senior Lecturer, Department of Language, Literature and Culture, Maasai Mara University

Keywords:

Utopia, Falsafa, Utandawazi, Kisaikolojia, Teknolojia

Abstract

Fasihi kama kioo cha jamii, huelimisha, huhifadhi tamaduni za jamii na pia kuadilisha.  Utafiti huu wetu ulifaidi kutoka kipengele cha fani kwa kuhakiki mtindo na mitazamo.  Daistopia ni jamii iliyochorwa na mwandishi wa kazi ya fasihi andishi na sifa kuu ya jamii hii lengwa ni kutozingatia maadili.  Utafiti huu ulihakiki utanzu wa riwaya ambao ulimulika daistopia kwa kina ili kuonyesha makuzi na maendeleo yake.  Utafiti huu ulihakiki  riwaya teule za Kiswahili  Kufa Kuzikana (2003), Dunia Yao (2006) na Chozi la Heri (2014).  Riwaya hizi ziliteuliwa kwa kusudi la kuafiki malengo mahsusi ya utafiti huu ambayo ni kuhakiki maudhui daistopia katika riwaya teule za kiswahili;  kutathmini mtindo uliotumika katika ujenzi wa daistopia katika riwaya teule na kuhakiki mitazamo ya daistopia katika riwaya hizi teule.  Ili kufanikisha utafiti huu tuliongozwa na nadharia ya Umitindo iliyoasisiwa naye Buffon (1930).   Nadharia hii ilikuwa kama dira katika kuzingatia mihimili yake ili kukusanya data mwafaka kukidhi malengo ya utafiti wetu.  Utafiti wetu ulikuwa wa maktabani.  Data ilikusanywa na kuwekwa katika makundi matatu makuu yanayoafiki malengo ya utafiti wetu.  Data ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu elezi na matokeo ya utafiti yatawasilishwa kwa njia ya kinathari.   Matokeo yalikuwa na mchango mkubwa katika fasihi ya lugha ya Kiswahili kwa kuwa yaliongezea maarifa kuhusu daistopia na jinsi imesawiriwa katika sanaa ya fasihi andishi katika lugha ya Kiswahili.

Published

2026-01-26

How to Cite

Syekei, M. N., Nyandiba, C., & Owala, S. (2026). Mitazamo ya Daistopia Katika Riwaya Teule za Kiswahili. African Journal of Advanced Social Sciences, 2(1). Retrieved from https://journals.evonexpublishers.com/index.php/ajass/article/view/59

Issue

Section

Articles