https://journals.evonexpublishers.com/index.php/ajass/issue/feedAfrican Journal of Advanced Social Sciences2026-01-20T06:00:43+00:00Managing Editorinfo@evonexpublishers.comOpen Journal Systems
African Journal of Advanced Social Sciences (AJASS) publishes peer-reviewed research in all areas of social and human sciences. It encourages interdisciplinary research, fosters an environment for cross disciplinary research connections and also accepts a range of article types including reviews, short communications and replication studies. Through hybrid open access publishing model, it aims at bringing research and knowledge to the widest possible audience.
https://journals.evonexpublishers.com/index.php/ajass/article/view/61Ulinganishi: Masimulizi Ya Jadi Ya Fasihi Simulizi: Chaka, Sundiata, Liyongo Na Mwindo Na Ya Kisasa2026-01-19T09:08:55+00:00Martha Nyangweso Syekeiondimumartha@yahoo.com
asihi imepitia mabadiliko kadha wa kadha katika hali ya kukua kwake. Mwanzo kulikuwa na fasihi simulizi – hadithi, semi, ngomezi, maigizo, ushairi simulizi na mazungumzo, kisha fasihi hii ikahifadhiwa kimaandishi na kuitwa fasihi andishi – tamthilia, riwaya, hadithi fupi na ushairi andishi. Baadaye fasihi ya kimajaribio imezuka ambayo wengi husema hii kati ya simulizi na andishi na ndiyo imesheheni karne hii mpya – fasihi ya watoto, vijana na watu wazima. Fasihi hii hutumia vigezo mbalimbali vya fasihi simulizi na andishi. Nadharia mbili zilizofaa makala haya ni za uhakiki wa vikale na nadharia ya uamilifu. Mihimili ya nadharia hizi mbili itaonyeshwa jinsi inavyojidhihirisha katika kazi hii ya fasihi. Yaliyomo yatafafanuliwa kwa kuongozwa na nadharia hizi, maelezo na ithibati yatatolewa kwa njia ya maelezo. Matokeo yatadhihirisha namna fasihi imekua na tofauti ya kale na sasa hasa vigezo za vya kutambua mashujaa.
2026-01-20T00:00:00+00:00Copyright (c) 2026 Martha Nyangweso Syekeihttps://journals.evonexpublishers.com/index.php/ajass/article/view/59Mitazamo ya Daistopia Katika Riwaya Teule za Kiswahili2026-01-19T08:57:07+00:00Martha Nyangweso Syekeiondimumartha@yahoo.comCarren Nyandibaondimumartha@yahoo.comSilas Owalaondimumartha@yahoo.com
Fasihi kama kioo cha jamii, huelimisha, huhifadhi tamaduni za jamii na pia kuadilisha. Utafiti huu wetu ulifaidi kutoka kipengele cha fani kwa kuhakiki mtindo na mitazamo. Daistopia ni jamii iliyochorwa na mwandishi wa kazi ya fasihi andishi na sifa kuu ya jamii hii lengwa ni kutozingatia maadili. Utafiti huu ulihakiki utanzu wa riwaya ambao ulimulika daistopia kwa kina ili kuonyesha makuzi na maendeleo yake. Utafiti huu ulihakiki riwaya teule za Kiswahili Kufa Kuzikana (2003), Dunia Yao (2006) na Chozi la Heri (2014). Riwaya hizi ziliteuliwa kwa kusudi la kuafiki malengo mahsusi ya utafiti huu ambayo ni kuhakiki maudhui daistopia katika riwaya teule za kiswahili; kutathmini mtindo uliotumika katika ujenzi wa daistopia katika riwaya teule na kuhakiki mitazamo ya daistopia katika riwaya hizi teule. Ili kufanikisha utafiti huu tuliongozwa na nadharia ya Umitindo iliyoasisiwa naye Buffon (1930). Nadharia hii ilikuwa kama dira katika kuzingatia mihimili yake ili kukusanya data mwafaka kukidhi malengo ya utafiti wetu. Utafiti wetu ulikuwa wa maktabani. Data ilikusanywa na kuwekwa katika makundi matatu makuu yanayoafiki malengo ya utafiti wetu. Data ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu elezi na matokeo ya utafiti yatawasilishwa kwa njia ya kinathari. Matokeo yalikuwa na mchango mkubwa katika fasihi ya lugha ya Kiswahili kwa kuwa yaliongezea maarifa kuhusu daistopia na jinsi imesawiriwa katika sanaa ya fasihi andishi katika lugha ya Kiswahili.
2026-01-26T00:00:00+00:00Copyright (c) 2026 Martha Nyangweso Syekei, Carren Nyandiba, Silas Owalahttps://journals.evonexpublishers.com/index.php/ajass/article/view/60Uhakiki wa Maudhui ya Daistopia Katika Riwaya Teule za Kiswahili2026-01-19T09:02:47+00:00Martha Nyangweso Syekeiondimumartha@yahoo.comCarren Nyandibaondimumartha@yahoo.comSilas Owalaondimumartha@yahoo.com
Fasihi kama kioo cha jamii, huelimisha, huhifadhi tamaduni za jamii na pia kuadilisha. Katika fasihi andishi vipengele vya fani na maudhui ndivyo vikuu. Utafiti huu wetu ulifaidi kutoka kipengele cha maudhui yalihakikiwa ili kuelezea mada yetu ya daistopia. Daistopia ni jamii iliyochorwa na mwandishi wa kazi ya fasihi andishi na sifa kuu ya jamii hii lengwa ni kutozingatia maadili. Utafiti huu ulihakiki utanzu wa riwaya ambao ulimulika daistopia kwa kina ili kuonyesha makuzi na maendeleo yake. Utafiti huu ulihakiki riwaya teule za Kiswahili Kufa Kuzikana (2003), Dunia Yao (2006) na Chozi la Heri (2014). Riwaya hizi ziliteuliwa kwa kusudi la kuafiki malengo mahsusi ya utafiti huu ambayo ni kuhakiki maudhui daistopia katika riwaya teule za kiswahili; kutathmini mtindo uliotumika katika ujenzi wa daistopia katika riwaya teule na kuhakiki mitazamo ya daistopia katika riwaya hizi teule. Ili kufanikisha utafiti huu tuliongozwa na nadharia ya Umitindo iliyoasisiwa naye Buffon (1930). Nadharia hii ilikuwa kama dira katika kuzingatia mihimili yake ili kukusanya data mwafaka kukidhi malengo ya utafiti wetu. Utafiti wetu ulikuwa wa maktabani. Data ilikusanywa na kuwekwa katika makundi matatu makuu yanayoafiki malengo ya utafiti wetu. Data ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu elezi na matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya kinathari. Matokeo yalikuwa na mchango mkubwa katika fasihi ya lugha ya Kiswahili kwa kuwa yaliongezea maarifa kuhusu daistopia na jinsi imesawiriwa katika sanaa ya fasihi andishi katika lugha ya Kiswahili.
2026-01-26T00:00:00+00:00Copyright (c) 2026 Martha Nyangweso Syekei, Carren Nyandiba, Silas Owala