Ulinganishi: Masimulizi Ya Jadi Ya Fasihi Simulizi: Chaka, Sundiata, Liyongo Na Mwindo Na Ya Kisasa

Authors

  • Martha Nyangweso Syekei Rongo University

Keywords:

Mighani, shujaa, kale, kisasa, masuala ibuka.

Abstract

asihi imepitia mabadiliko kadha wa kadha katika hali ya kukua kwake.  Mwanzo kulikuwa na fasihi simulizi – hadithi, semi, ngomezi, maigizo, ushairi simulizi na mazungumzo, kisha fasihi hii ikahifadhiwa kimaandishi na kuitwa fasihi andishi – tamthilia, riwaya, hadithi fupi na ushairi andishi.  Baadaye fasihi ya kimajaribio imezuka ambayo wengi husema hii kati ya simulizi na andishi na ndiyo imesheheni karne hii mpya – fasihi ya watoto, vijana na watu wazima.  Fasihi hii hutumia vigezo mbalimbali vya fasihi simulizi na andishi.  Nadharia mbili zilizofaa makala haya ni za uhakiki wa vikale na nadharia ya uamilifu.  Mihimili ya nadharia hizi mbili itaonyeshwa jinsi inavyojidhihirisha katika kazi hii ya fasihi.  Yaliyomo yatafafanuliwa kwa kuongozwa na nadharia hizi, maelezo na ithibati yatatolewa kwa njia ya maelezo. Matokeo yatadhihirisha namna fasihi imekua na tofauti ya kale na sasa hasa vigezo za vya kutambua mashujaa.

Published

2026-01-20

How to Cite

Syekei, M. N. (2026). Ulinganishi: Masimulizi Ya Jadi Ya Fasihi Simulizi: Chaka, Sundiata, Liyongo Na Mwindo Na Ya Kisasa. African Journal of Advanced Social Sciences, 2(1). Retrieved from https://journals.evonexpublishers.com/index.php/ajass/article/view/61

Issue

Section

Articles